Druckansicht der Internetadresse:

Cluster of Excellence EXC 2052 - "Africa Multiple: reconfiguring African Studies"

Print page

Kitengo cha Utafiti kwa Muhtasari

Kitengo cha Utafiti kwa Muhtasari

Kitengo-anuwai kinachoangazia utafiti katika Taaluma za Afrika ambacho kilianzishwa mnamo Januari 2019 kupitia Mkakati Maalum wa Ushurikiano wa Serikali ya Ujerumani, kwa kujenga rekodi ndefu na ya kifahari katika Taaluma za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Bayreuth, kinazingatia maazimio na ajenda ya uvumbuzi, iliyoelezwa katika mada ndogo "Uwazaji-Upya katika Taaluma za Kiafrika". Awali kilijumuisha Wachunguzi Wakuu ishirini na watano, hata hivyo idadi hiyo imekuwa ikiongezeka. Kwa sasa kitengo hicho cha utafiti kinawahusisha zaidi ya wasomi na watafiti zaidi ya mia moja kutoka mabara matatu, ambao wanawakilisha nyuga tofauti za kitaaluma. Watafiti hao hushirikiana katika kufanya tafiti zinazoingiliana pamoja na taasisi zinazoshirikiana kitaaluma katika Afrika, Ujerumani, Ulaya, Asia na Marekani.

Zaidi ya Mabadiliko ya Ki-Mtazamo
Uelewa wetu wa Uwazaji-Upya wa Taaluma za Kiafrika unajikita katika kuchochea mikabala mipya ya kinadharia na unajumuisha uundaji mpya wa ushirikiano wa kitaaluma. Washiriki lengwa sio tu kutoka Chuo Kikuu cha Bayreuth, lakini pia wanatoka kwenye taasisi za kitaaluma kutoka Afrika na kwingineko. Watafiti hao hufanya tafiti na kuibua maswali ya utafiti pamoja na  kushirikisha nadharia katika miradi ya taaluma mbalimbali, nyingi ya hizo ni zile hasa zinazoendeshwa pamoja na Vituo vya Tafiti Afrika (ACCs) katika Chuo Kikuu cha Joseph Ki-Zerbo (Burkina Faso), Chuo Kikuu cha Lagos (Nigeria), Chuo Kikuu cha Moi (Kenya), Chuo Kikuu cha Rhodes (Afrika Kusini) na Kituo cha Taaluma ya Afro-Asia katika Chuo Kikuu cha Bahia, Brazil  (Federal University of Bahia, Brazil).

Kuunda Nafasi ya Mabadiliko kwenye Taaluma za Kiafrika
Kupitia Bayreuth Academy of Advanced African Studies, Kitengo hiki cha utafiti huendesha mpango wa Mbadilishano wa watafiti Chipukizi na Waandamizi ambao hushiriki kufuatia mwaliko na pia kutokana na wito wa kimataifa unaotolewa mara kwa mara. Taasisi hiyo pia inatoa muundo maalum kwa ajili ya mafunzo ya watafiti waliokamilisha uzamifu na kuratibu makundi manne huru ya Watafiti Chipukizi wanaofanya tafiti zinazoingiliana na Taaluma za Kiafrika. Mafunzo yenye mwelekeo wa utafiti wa baada-uzamifu hutolewa kupitia Bayreuth International Graduate School of African Studies (BIGSAS), iliyoanzishwa mwaka 2007. Kadhalika, BIGSAS hutoa rasilimali kuu kwa kitengo hiki cha utafiti chenye mtandao mkubwa wa ushirikiano wa watafiti na wanafunzi wa zamani zaidi ya 200 ambao ni chipukizi na pia wataalamu waliobobea. Kituo kinachojulikana kimataifa kama Iwalewahaus (kilichoanzishwa mnamo 1981), ni kituo maarufu kinachojihusisha na sanaa ya Kiafrika, na huchangia pakubwa kazi zetu kupitia maonyesho, nyaraka, utafiti na mifumo inayojumuisha nyuga anuwai na wasanii mbalimbali. Wahusika wote katika kitengo cha utafiti, wawe wanatoka Bayreuth, Afrika, au kwingineko duniani, wameunganishwa na Mazingira yetu ya Utafiti wa Ki-Dijitali (Digital Research Environment-DRE). DRE inaunganisha data nyingi za ki-analogi na ki-dijitali, za kitaamuli na kitakwimu katika jukwaa la kawaida la utafiti wa kidijitali. Jambo hili hutupa fursa kushirikisha data na kutoa muundo wa kufanya kazi zinazoonyesha utofauti, uthakili na mabadiliko ya utafiti pamoja na madhumuni yanayolenga kuanzisha uvumbuzi wa teknolojia na ontolojia za Teknolojia ya Habari. Kitengo hiki cha utafiti kinalenga kukuza fursa sawa na utambuzi wa utofauti kupitia Ofisi ya Jinsia na Utofauti (GDO) kupitia utetezi wake wa Makutano na Mitazamo Anuwai ya Kusoma (ICDL). GDO imejumuishwa katika mazingira ya muumano baina ya utafiti na utawala. Isitoshe, GDO imewekezwa kwenye maendeleo na utekelezaji wa hatua za kusawazisha changamoto za kimiundo, pamoja na kuimarisha mbinu za utafiti kupitia mwingiliano wa ki-taaluma.

Dhana Mpya na Miundo ya Utafiti
Dhana kuu zinazoangaziwa ni nyumbufu-tafiti, uhusiano-tafiti, na uakisi-tafiti. Tunazitumia dhana hizi ili kubaini uhusiano unaobadilika wa uanuwai na ambao ni sifa ya maisha ya Mwafrika na hali ya Uafrika Ughaibuni pamoja na uumbaji wa ulimwengu.  Katika Maabara ya Maarifa, msingi wa taaluma katika kitengo cha utafiti unaunganisha masuala yetu ya kinadharia, kiepistemolojia, na mbinu za utafiti, uibuaji wa mijadala pevu ya kitaaluma na kuchochea maelewano na maendeleo mapya ya kinadharia.  Sehemu sita za mada, zilizopangwa katika Vitengo vya Utafiti, hutoa kwa umadhubuti muundo wa miradi yetu ya utafiti. Miradi mingi huendana na/au ajenda ya taaluma zinazojumuisha nyuga mbalimbali na pia huhusisha ushirikiano wa karibu kati ya watafiti kutoka Bayreuth, Afrika, na mtandao wetu wa kimataifa.


Webmaster: Olutosin Akinwumi

Facebook Twitter Youtube-Kanal Instagram UBT-A